NATO Yasema China Ni Changamoto Kwa Usalama Wao

 

Mkuu wa muungano wa Nato amewataka wanachama wa muungano huo kuzungumzia kuhusu kuimarika kwa China katika mkutano ulioitishwa ili kuonesha jinsi Marekani inavyounga mkono muungano huo wa mataifa ya Magharibi.

Mkutano huo unatarajiwa kutoa taarifa inayoelezea tabia za China kama Changamoto kuu baada ya mkutano huo nchini Ubelgiji.

Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alisema kwamba mkutano huo ulikuwa muhimu kwa muungano huo.

Ni mkutano wa kwanza wa rais wa Marekani Joe Biden tangu alipochukua madaraka.

Nato ni muungano wenye uwezo mkubwa kisiasa na kijeshi kati ya mataifa 30 ya magharibi pamoja na yale ya Marekani kaskazini.

Ulibuniwa baada ya vita ya pili ya dunia ili kujibu kupanuka kwa uongozi wa kikomyunisti.

Katika miaka ya hivi karibuni , Muungano huo ulikumbwa na changamoto wakati viongozi walipojadili kuhusu lengo lake na ufadhili.

Hali ya wasiwasi iliongezeka wakati wa utawala wa rais Trump ambaye alilalamika kuhusu ufadhili wa taifa lake na kuhoji jukumu la Marekani kutetea washirika wake wa Ulaya.

Badala yake , mrithi wake Bwana Biden ametaka kuimarisha uungwaji mkono wa Marekani kwa muungano huo wenye takriban miaka 72.

''Nataka kuweka wazi : Nato ni muhimu sana kwa maslahi ya Marekani'' , bwana Biden alisema alipowasili katika mkutano huo siku ya Jumatatu.

Taifa lake lilisema kwamba, lilikuwa na jukumu la siri kuafikia kifungu cha 5 cha makubaliano ya Nato , ambayo yanashurutisha mataifa wanachama kujilinda dhidi ya mashambulizi.


EmoticonEmoticon