Raisi Wa Marekani Asema Kila Atakayechomwa Chanjo Alipwe Zaidi Ya Laki 2

 

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kila mwananchi atakaekubali kupigwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 atalipwa dola 100(Laki 2). Marekani ni nchi yenye chanjo za kutosha na idadi kubwa ya watu wanaopinga kuchanjwa.

Rais wa Marekani Joe Biden amewashauri Viongozi wa Majimbo na Miji yote nchini humo kuwalipa wakazi wao Dola 100 ili wapigwe chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Aidha ameweka sheria mpya zinazohitaji wafanyakazi wote wa Serikali kuonyesha uthibitisho wa kupigwa chanjo au kulazimika kupimwa ugonjwa huo mara kwa mara, kuvaa barakoa pamoja na kuwekewa vikwazo vya kusafiri.

Hatua hizo za hivi karibuni ni miongoni mwa juhudi za Biden kujaribu kuwahamasisha Wamarekani wenye kupiga chanjo, huku aina mpya ya virusi vya corona iitwayo Delta ikiwa inaenea kote nchini humo, hasa miongoni mwa watu ambao bado hawakuchanjwa.