Askari 19 Kutoka Kikosi Maalum Nigeria Wauawa Katika Shambulizi La Kushtukiza

 

Jeshi la Nigeri limepoteza wanajeshi 19 wa kikosi maalum kinacholinda eneo la Torodi, kati ya Niger na mpaka wa Burkina Faso. Mashambulio mawili yalitekelezwa na watu wenye silaha.

Eneo la mipaka mitatu, hususan lile la eneo la bustani ya watalii, mara kwa mara linakabiliwa na mashambulio ya kigaidi. Jeshi limekuwa linaendesha operesheni la kuwasaka washambuliaji katika eneo hili kwa saa 48 sasa.

Wanajeshi hawa walikuwa katika ujumbe wa kusafirisha chakula katika kituo cha Boni, katika eneo la Torodi, walishambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana.

Kulingana na taarifa kutoka Baraza la kitaifa la ulinzi, idadi ya wanajeshi19ni kubwa sana: wanajeshi 15 walifariki, saba wamejeruhiwa na sita hawajulikani waliko. Hata hivyo Wizara ya Ulinzi imebaini kwamba wanajeshi 19 na raia mmoja ndio waliuawa.

Wanajeshi hawa waliouawa wote ni kutoka kikosi cha Operesheni Saki II, kikosi maalum kinacholinda eneo hili la mipaka mitatu, karibu kilomita zaidi ya mia moja kusini magharibi mwa Niamey.