Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano September 22

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano September 22

1. Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial atakuwa huru kuondoka Manchester United katika dirisha la usajili la Januari. Mchezaji huyo wa miaka 25 yuko huru kukaa katika Ligi ya Premia lakini anaweza kutafuta fursa barani, na Barcelona inaweza kuwa chaguo.

2. Chelsea wanaandaa ofa mpya za mkataba wa kiungo wa England Mason Mount, 22, kiungo wa Ufaransa N'Golo Kante, 30, na kiungo wa Italia 29, Jorginho. 

3. Chelsea walikuwa tayari kutoa euro milioni 100 (pauni milioni 86) kwa ajili ya mlinzi wa Paris St-Germain na mlinzi wa Brazil Marquinhos, 27, katika majira ya joto.

4. Manchester City wanafuatilia fowadi wa Real Sociedad na Uhispania Mikel Oyarzabal, 24.

5. Barcelona wanajiandaa kuachana na kocha mkuu Ronald Koeman, huku bosi wa Ubelgiji Roberto Martinez akiwa "chaguo bora" kuchukua nafasi ya Mholanzi huyo.