Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi September 23

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi September 23

1. Chelsea wanataka kumsajili beki wa kati wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22. 

2. Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu. 

3. Barcelona italazimika kulipa euro milioni 1.8 (£ 1.5m) ili kumtoa Roberto Martinez kutoka kwa mkataba wake na timu ya taifa ya Ubelgiji. 

4. Bayern Munich wana nia ya kumsajili beki wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, lakini mchezaji huyo wa miaka 28 anataka kusaini mkataba mpya huko Stamford Bridge. 

5. Liverpool wanamtazama winga wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 25.