Kesi Ya Zuma Kuunguruma Leo Mahakamani

 

Kesi ya rushwa inayomhusisha rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma inapaswa kuanza tena leo.

Kesi hiyoimecheleweshwa mara kwa mara, hivi karibuni kwa sababu Bwana Zuma alikuwa amelazwa hospitalini kwa hali ya kiafya isiyojulikana.

Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo, na anasisitiza kuwa maadui zake wa kisiasa wanatumia korti kumlenga. Kukamatwa kwake kulisababisha wiki kadhaa za machafuko nchini humo na kusababisha uporaji wa mali na maafa .