Raisi Wa Marekani Ahutubia Hadhara Kuu Ya Umoja Wa Mataifa

 

Rais Joe Biden wa Marekani ameitaka dunia kuongeza nguvu katika kukabiliana na janga la Covid-19, mabadiliko ya tabia nchi na ukiukwaji wa haki za binaadamu. 

Katika hotuba yake ya kwanza ya ufunguzi,Joe Biden amezungumzia migogoro ya kijeshi na kuongeza pia, Marekani haitafuti vita mpya baridi na hasimu wake wa kibiashara China.

Wakati akiwasisitiza viongozi wenzake umhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano, Biden ameonekana kukwepa kujibu ukosoaji kutoka kwa washirika wake juu ya namna tata ya Marekani ilivyojiondoa Afghanistan na tofauti za sasa kidiplomsia na Ufaransa.

Lakini badala yake alitumia jukwaa hilo la kila mwaka kusema Marekani itaendelea kuwa mshirika wa kutegemewa wa kimataifa baada ya kile alichokisema sera ya mambo ya nje ya mtangulizi wake, Donald Trump ya Marekani kwanza. 

Kuhusu makabiliano ya mabadiliko ya tabia nchi Biden ametoa ahadi ya msaada wa mataifa masikini wa dola bilioni 11.4 kwa mwaka."Mwezi Aprili nilitangaza kwamba Marekani itaongeza mara mbili msaada wetu wa kifedha, katika kusaidia mataifa yanayoendelea kukabiliana na janga la kimazingira na leo najivunia kutangaza, tutatafanya kazi na bunge la Marekani, kuongeza idadi hiyo mara mbili tena, zikiwemo juhudi za kukabiliana." alisema kiongozi huyo.