Waziri Wa Ulinzi Lithuania Aonya Watu Kuacha Kununua Simu Za China

 

Watumiaji wanastahili kutupa simu zao za China na kujizuia kununua simu mpya, Waziri wa Ulinzi wa Lithuania ameonya.

Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Usalama wa Taifa wa Kimtandao, imesema imefanya majaribio ya simu za mkononi za 5G kutoka kwa watengenezaji wa China.

Na kudai kuwa simu ya Xiaomi ilikuwa imejumuishwa king'amuzi au kidhibiti wakati inatengenezwa kwa ndani huku simu nyingine aina ya Huawei ikiwa na mapungufu ya kiusalama.

Kampuni ya Huawei imesema kwamba hakuna data ya mtumiaji iliyoelekezwa kwengineko huku simu ya Xiaomi nayo ikisema kwamba sio kweli eti inachunguza mawasiliano ya watu.

"Mapendekezo yetu ni kwamba musinunue simu mpya za China, na pia muachane na zile ambazo tayari mumeshanunua haraka iwezekanavyo," amesema Naibu Waziri wa Ulinzi Margiris Abukevicius.