Mafuriko Yasababisha Vifo Vya Watu Zaidi Ya 20 India

 

Watu wasiopungua 24 wamefariki katika mafuriko kusini mwa India baada ya mvua kubwa kusababisha mito kufurika, kukata usafiri katika miji na vijiji.

Watoto watano ni kati ya waliokufa.

Kuna hofu idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka zaidi kwani watu wengi hawajulikani waliko.

Nyumba kadhaa zilisombwa na maji na watu walinaswa katika wilaya ya Kottayam katika jimbo la Kerala.

Video kutoka eneo hilo ilionyesha abiria wa basi wakiokolewa baada ya gari lao kujaa maji ya mafuriko. Kottayam na Idukki ni wilaya mbili zilizoathirika zaidi katika jimbo hilo.

Siku kadhaa za mvua kubwa pia zimesababisha maporomoko hatari ya ardhi.