Ufaransa Yazindua Magari Ya Umeme Nchini Tanzania

 

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion Africa.

Kampuni ya E-Motion Africa iliundwa mnamo 2019 kwa lengo la kutoa suluhisho la asili na rahisi kwa changamoto ya usafiri unaotoa gesi ya kaboni nchini Tanzania na inapendekeza kubadilisha injini ya dizeli ya magari ya uchukuzi kuwa magari ya umeme, unayotumia na nguvu ya betri.

Kwa mujibu The Citizen nchini Tanzania, Waziri Riester amenukuliwa akisema “Gari lisilotoa gesi chafu ndio gari la siku zijazo”.

Pia alisema Ufaransa imejitolea kukuza ushirikiano na kushirikiana kiteknolojia na Tanzania.

Mradi huo ulianzishwa na kampuni ya safari ya Ufaransa Mount Kilimanjaro Safari Club (MKSC) ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa miaka 20 kaskazini mwa nchi katika mbuga za kitaifa.

Credit : Bbc