Apigwa Marufuku Kuingia Kwenye Mgahawa Kwa Kula Chakula Kupita Kiasi

 

Mwanaume mmoja wa Uchina anasema amewekwa kwenye orodha ya ‘’nyeusi’’ na mgahawa mmoja wa chakula kwasababu ana uwezo wa kula chakula kingi kwa mpigo.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Bw Kan, aliiambia televisheni ya Hunan TV kwamba amepigwa marufuku kuingia katika mgahawa unaojulikana kama Hunter's seafood restaurant uliopo Changsha baada ya kula mlo katika mgahawa huo.

Mara ya kwanza nilipoenda kwenye mgahawa, nilikula nusu kilo ya miguu ya nguruwe na mara ya pili nikala kilo nne za uduvi.

Bw Kan amelalamika kuwa mgahawa huo unaubaguzi dhidi ya watu wanaokula chakula kingi kupita kiasi.

"Ni dhambi kupita kiasi?, Nini tatizo? Hakuna chakula nilichobakiza kilichoharibika."

Lakini mmiliki wa mgahawa anasema Bw Kanamekuwa akimsababishia hasara.

"Kila wakati anapokuja hapa, napoteza mamia ya pesa -won," alisema.

"Hata kama akinywa maziwa ya soya, anaweza kunywa vikombe 20 au 30. Kama anakula miguu ya nguruwe , anaweza kula sahani nzima iliyojaa ya uduvi.

"Kwa upande wa uduvi, wengine hutumia mkasi. Lakini yeye huwa anakula sahani kubwa nzima na kujaza uduvi indani yake," alisema.

Aliongeza kuwa sio watu wote watakaokuwa wakiruhusiwa kutembelea mgahawa huo kushiriki chakula cha jioni.

Taarifa hii imeibua maoni tofauti kwenye mitandao ya kijamii ya Uchina, huku taarifa hii ikitazamwa na watu milioni 250 katika mtandao wa Weibo.

Baadhi ya watu wanasema kuwa mgahawa huo haupaswi kufunguliwa kwa ajili ya chakula kama hauwezi kutoa chakula cha kutosha kwa kila mtu, huku wengine wakimuonea huruma mmiliki wa mgahawa.

Tukio hili linakuja huku rais wa Uchina Xi Jinping akiwataka watu kutoharibu chakula kutokana na hofu ya upungufu wa chakula nchini humo.