Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne November 23

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne November 23, 2021

1. Wachezaji wa klabu ya Paris St-Germain wanaamini kwamba Mauricio Pochettino ataondoka kuelekea Manchester United huku raia wa U faransa Zinedine Zidane akimrithi katika klabu ya PSG. 

2. Manchester United italazimika kulipa Yuro Milioni 10 (£8.4m) iwapo wanataka kumnunua raia wa Argentina Pochettino mwenye umri wa miaka 49 kutoka klabu ya PSG.

3. Mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah anakaribia kuandikisha kandarasi ya muda mrefu katika klabu hiyo. Mchezaji huyo ataingia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake msimu ujao huku klabu hiyo ikijiandaa kukamilisha masharti mapya ya mkataba wake.

4. West Ham wanafanya bidi kumsaini mshambuliaji wa Sparta Prague na Czech Republic Adam Hlozek, 19.

5. Barcelona huenda ikafutilia mbali kandarasi ya mchezaji Samuel Umtiti. Beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 ameshindwa kukubali pato lililopunguzwa kwa mshahara wake wa £208,000 kwa wiki huku klabu hiyo ikikabiliwa na matatizo ya kifedha.