Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano November 24

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano November 24, 2021

1. Manchester United wako tayari kuacha utafutaji wa meneja wa muda wa klabu hiyo iwapo wanaweza kumpata Mauricio Pochettino kutoka Paris St-Germain sasa. 

2. Meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, ambaye ana uwezekano mkubwa wa kulengwa na Manchester United anataka kuchukua umeneja katika PSG iwapo Pochettino anaondoka kuelekea Old Trafford. 

3. Borussia Dortmund wana andaa mkataba mpya kwa ajili ya mshambuliaji Erling Braut Haaland, 21, katika azma ya kumshawishi mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway kuendelea kubaki katika klabu hiyo. 

4. Barcelona wanamtafuta mchezaji wa wa kimataifa wa Morocco anayechezea klabu ya Chelsea Hakim Ziyech, 28, na mshambuliaji Mjerumani Timo Werner, 25, kama wachezaji mbadala kwa mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 26. 

5. Liverpool, Leicester na Newcastle wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Guinea Aguibou Camara mwenye umri wa miaka 20, anayecheza katika klabu ya Olympiakos.