Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi November 25

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi November 25, 2021

1. Mshambuliaji wa Paris St-Germain na France Kylian Mbappe, 22, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo wakati kandarasi yake itakapokwisha msimu wa ujao , huku Newcastle united ikiwa miongoni mwa klabu ambayo inawaza kumuwania mchezaji huyo mshindi wa kombe la dunia.

2. Wito wa Manchester United kutaka kumuajiri mkufunzi wa klabu ya PSG Mauricio Pochettino umekataliwa na klabu hiyo. Meneja huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham Pochettino , 49 atalazimika kusubiri miezi sita kabla ya kuweza kuwa mkufunzi wa Man United.

3. Picha ya aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United Olegunnar Solskjaer imeondolewa katika uwanja wa Old Trafford. 

4. Liverpool na Barcelona zinamuwania mshambuliaji wa Chelsea Christian Pulisic, 23, lakini The Blues haiwezi kumuuza mchezaji huyo kwa timu yoyote ya Ligi ya Premia huku klabu hiyo ya Uhispania ikiwa haina uwezo wa kutoa dau la Yuro 50m linalohitajika ili kumsaini winga huyo wa Marekani.

5. Mashabiki wa Real Madrid wamemkera mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, kulingana na ajenti wake Jonathan Barnett. Bale, 32, ana kandarasi na Real Madrid hadi majira yajayo ya joto.