Sindano Ya UKIMWI Yaidhinishwa

 

Maelfu ya watu wanaoishi na virusi vya HIV sasa watakuwa wanapewa sindano mpya yenye ufanisi wa muda mrefu ili kudhibiti hali zao iwapo watataka kuacha kumeza vidonge kila siku.

Mashirika ya misaada yameafiki idhini hii ya matibabu ya taasisi ya usimamizi wa madawa nchini Uingereza NHS nchini Uingereza.

Sindano hii husitisha makali ya virusi, sawa na dawa za kawaida za antiretroviral .

nakadiriwa kuwa watu 13,000 nchini Uingereza wanaweza kuamua kudungwa sindano hiyo badala ya vidonge.

Dawa hiyo ya sindano inayofahamika kama Cabotegravir (pia ikiitwa Vocabria na kutengenezwa na ViiV Healthcare) na rilpivirine (pia ikiitwa Rekambys na kutengenezwa na Janssen) hutolewa kama sindano mbili tofauti kila baada ya miezi miwili.

Tiba hiyo ni bora tu kwa wale ambao wameweza kufanikiwa kufikia viwango vya kutogundulika kwa virusi katika damu yao wakati wanapomeza vidonge.

Wataalamu wanasema tiba hii ya sindano inaweza kuwa rahisi kutumiwa na wengi.