Waziri Mkuu Wa Kwanza Mwanamke Sweden Ajiuzulu

 

Waziri mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa kadhaa tu baada ya kuteuliwa.

Magdalena Andersson, alitangazwa kama kiongozi Jumatano, lakini alijiuzulu baada chama kishiriki katika muungano wake kujiuzulu serikalini na bajeti yake kushindwa kupitishwa.

Badala yake, bunge lilipigia kura bajeti iliyoandaliwa na upinzani ambayo ilijumuisha mpango wa mrengo wa kulia zaidi wa kupinga uhmiaji.

"Nimemwambia spika kwamba ningependa kujiuzulu ,"Bi Anderssonaliwaambia waandishi wa habari.

Mshirika wake katika muungano, chamba cha kijani (Greens Party) kilisema kuwa kuwa hakikuweza kuikubali bajeti "iliyoandaliwa kwa mara ya kwanza na cha upinzani cha mrengo wa kulia zaidi ".

Bi Andersson alisema kwamba ana matumaini ya kujaribu kuwa waziri mkuu tena kama kiongozi wa serikali wa chama kimoja.