Wazungu Watatu Wapatikana Na Hatia Ya Mauaji Ya Mtu Mweusi

 

Wanaume watatu wamepatikana na hatia ya kumuua mtu mweusi aliyekuwa akijfanya mazoezi kukimbia mwaka jana katika kesi ambayo iligeuka kuwa kilio cha kudai haki ya rangi ya waandamanaji.

Ahmaud Arbery, mwenye umri wa miaka 25 alipigwa risasi na kuuawa Februari 2020 katika makabiliano na Travis na Gregory McMichael na jirani wake, William Bryan.

Wanaume hao walijitetea kwa kusema kuwa walichukua hatua ya kumpiga risasi katika kujilinda , lakini waendesha mashitaka walisema rangi ilikuwa ni sababu ya kumpiga risasa.

Wanaume hao sasa wanakabiliwa na hukumu za kifungo cha maisha jela.

Jopo la mahakama lililoundwa na jumla ya wazungu 12 liliketi kutathmini kesi hiyo kwa saa 10 kabla ya kurejea kutoa hukumu takriban saa sita za mchana Jumatano.

Watatu hao walipatikana na hatia ya mauaji, kufanya shambulio kali, kusema uongo na kuazimia kutekeleza uhalifu kwa makusudi .

Mwezi Februari wanaume hao watatu watakabiliwa na mashitaka mengine katika kesi ya mahakama ya shirikisho kuhusiana na uhalifu wa chuki , kwa madai kuwa walimlenga Arbery kwasababu alikuwa mtu mweusi.

Story Kamaili : BBC SWAHILI