Zinedine Zidane Apiga Chini Deal La Manchester United

 

Manchester United inamtaka Zinedine Zidane awe meneja wao mpya, lakini kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na kocha huyo wa zamani wa Real Madrid, hana mpango wa kwenda Old Trafford.

Ole Gunnar Sskjaer alitimuliwa na Unites Jumapili baada ya kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Watford.

Zidane hana timu tangu aondoke Real manager mwezi Mei mwaka huu.

Ameshinda mataji matatu mflulizo ya ligi ya mabingwa Ulaya kuanzia mwaka 2016.

Baada ya kuondoka mara ya kwanza mwaka 2018, airejea mwaka mmoja baadae na kushinda taji la ligi kuu La Liga na kombe la Hispania la Super Cup mwaka 2020.

Chnajo hicho hicho kimesema kuwa kiungo huyo gwiji wa Ufaransa na Real Zidane, ambaye hana timu sasa, hana mpango wa kujiunga na United kwa sasa.

Amekuwa akihusishwa na timu ya taifa ya Ufaransa na Paris St-Germain, na angependelea kuchangamkia nafasi za kuongoza timu hizo, fursa ikitokea.