ASHTAKIWA KWA KUTAKA KUMUUA DONALD TRUMP

Mkazi wa Rockaway Beach, New York, nchini Marekani ameshtakiwa kwa tuhuma za kutaka kumuua Rais wa zamanı wa Marekani, Donald Trump. 

Baba huyo mwenye umri wa miaka 72 aitwae Thomas Welnicki, alifikishwa Mahakamani Jumatatu kusomewa shtka hilo.

Mshtakiwa huyo inaelezwa January 2021 alifanya mahojiano ya hiari huku akisema endapo Trump atashindwa Uchaguzi basi atamdhibiti kwa silaha.

Jarida la Complex liliripoti kwamba mtuhumiwa anashtakiwa kwa kukusudia na kutaka kumdhuru Rais wa Zamani.

Hata kama Trump hakutajwa kwa majina kwenye nakala hizo za Polisi, maelezo yalijitosheleza kuonyesha kuwa ni yeye ndio alikuwa anatishiwa maisha.