BEI YA MAHINDI HAISHIKIKI MASOKONI

 

Bei ya mahindi katika masoko mbalimbali mikoa ya Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara), haikamatiki huku bidhaa hiyo ikianza kuadimika.

Baadhi ya wakazi wa mikoa hiyo waliozungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, wameiomba serikali kupitia Wizara ya Kilimo, kupeleka haraka mahindi ya bei nafuu yaliyohifadhiwa katika Ghala la Taifa la Chakula (NRFA).

Uchunguzi wa Nipashe katika mikoa hiyo umebaini kupanda kwa bei ya mahindi kwa uwiano tofauti. Kupaa kwa bei hiyo kulianza kutikisa tangu mwishoni mwa mwaka jana, kutokana na kupungua sokoni.