HABARI KUBWA ZA SOKA ULAYA ALHAMISI JANUARY 13

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi January 13, 2022

1. Paris St-Germain wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, huku Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 28 pia akitaka kuhamia klabu hiyo ya Ligue 1. 

2. Wakati huo huo meneja wa PSG Mauricio Pochettino bado anawasiliana na Man Utd kuhusu uhamisho wa majira ya joto. Meneja wa sasa wa muda Ralf Rangnick, hata hivyo, anamtaka bosi wa Ajax Erik ten Hag. 

3. Beki wa Chelsea Antonio Rudiger sasa anapanga kusalia Stamford Bridge. Mjerumani huyo, 28, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao alikuwa akihusishwa na kutaka kuondoka. 

4. Manchester United wanamtaka beki wa kulia wa Brighton, Tariq Lamptey. Brighton wanataka pauni milioni 40 kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye ameichezea timu ya U-21 ya Uingereza. 

5. Juventus wana nia ya kutaka kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Barcelona na Uholanzi Memphis Depay, 27.