HABARI KUBWA ZA SOKA ULAYA JUMANNE JANUARY 11

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne January 11, 2022

1. Mshambulizi wa Uruguay Edinson Cavani, 34, ameahidi kujitolea kwa Manchester United kwa muda wote uliosalia wa msimu huu baada ya mazungumzo na mkufunzi Ralf Rangnick. 

2. Manchester City wanaweza kumfuatilia nahodha wa Croatia Luka Modric, ambaye hajafurahishwa na kuongezwa kwa mkataba unaotolewa na Real Madrid. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 katika klabu hiyo ya Uhispania unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

3. Mlinzi wa Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 28, ambaye mkataba wake unamalizika msimu wa joto na bado hajasaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Ulaya, anasemekana kupendelea kuhamia Real Madrid kuliko Paris St-Germain ikiwa ataondoka Stamford Bridge. 

4. Arsenal wako tayari kufadhili mkataba wa pesa nyingi kumsajili mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21 kutoka Fiorentina mwezi Januari. 

5. Paris St-Germain, AC Milan, Roma, Lyon, Barcelona na Newcastle United ni miongoni mwa vilabu ambavyo vinaweza kumtaka kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 25, ambaye mustakabali wake Tottenham haujulikani baada ya kuzomewa na mashabiki wa Spurs wakati alipolishwa benchi wakati wa Ushindi wa Jumapili wa Kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Morecambe.