HABARI KUBWA ZA SOKA ULAYA JUMATATU JANUARY 10

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu January 10, 2022

1. Mshambulizi wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, 23, bado anaweza kukataa kuhamia Real Madrid na kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. 

2. Mchezaji aliyesajiliwa kwa kiasi cha kuvunja rekodi Tanguy Ndombele, kiungo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25, ana matumaini ya kuondoka Tottenham Hotspur mwezi huu. 

3. Mshambulizi wa Bayer Leverkusen na Jamhuri ya Czech Patrik Schick, 25, anasema ana furaha katika klabu hiyo ya Bundesliga licha ya uvumi kuhusu kuhama mwezi Januari. 

4. Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel amependekeza kiungo wa kati wa Uingereza Ross Barkley, 28, anaweza kuruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo mwezi huu. 

5. Newcastle United wamewasiliana na Burnley kumnunua mshambuliaji wa New Zealand Chris Wood, 30.