WIMBI LA NNE LA CORONA LIMEFIKIA KILELENI BARANI AFRICA-WHO

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO limesema kasi ya maambukizi ya virusi vya corona aina ya omicron inaanza kupungua barani Afrika, baada ya wiki kadhaa za kusambaa kwa haraka. 

Mkurugenzi wa shirika hilo anayehusika na hali ya dharura kiafya barani Afrika, Abdou Salam Gueye amesema Afrika inaondokana na kitisho cha wimbi la nne la covid-19. 

Aidha, afisa huyo amesema maambukizi yamekuwa yakipanda kwa kasi kwa wiki sita mfululizo lakini sasa kasi hiyo inashuka.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, wimbi hili la nne ndilo lililodumu kwa muda mfupi zaidi barani Afrika. Hata hivyo, ameonya kuwa viwango vya watu waliopokea chanjo Afrika vinabaki kuwa vya chini.