ZAIDI YA WATU 20 WAFARIKI KWA BARIDI PAKISTAN

Takriban watu 21 wamekufa baada ya gari yao kukwama kwenye theluji nchini Pakistan. 

Waziri wa mambo ya ndani Sheikh Rashid Ahmed amesema tayari wamepeleka wanajeshi ili kusafisha barabara. 

Theluji hiyo imesababishwa na baridi kali katika mji wa kitalii ulioko maeneo ya milimani wa Murree. 

Waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan ameelezea kushtushwa na vifo hivyo na kuagiza uchunguzi lakini pia kuwekwa kwa kanuni kali za kuhakikisha majanga kama hayo hayatokei. 

Idadi kubwa ya watu wamekwama kwenye magari yao kuanzia watalii hadi wakazi wa mji huo.